Back to top

Geti kuu la forodha ya Tunduma na Nakonde lafungwa.

24 March 2019
Share

Geti kuu la forodha ya Tunduma na Nakonde limefungwa kwa muda baada ya raia wa Zambia kuzua vurugu mpakani wakishinikiza kuachiliwa huru kwa raia wenzao wa Zambia wanaoshikiliwa na polisi upande wa Tanzania waliokamatwa kwa tuhuma za uhalifu.

Shughuli za kiforodha zimaesimama kwa muda, maduka yamefungwa huduma za usafiri zimesimama, mpaka hali ya utulivu itakapopatikana ambapo hivi sasa viongozi wa jeshi la polisi kwa upande wa Tanzania na Zambia wapo katika mazungumzo.

Baada ya raia wa Zambia kuzua vurugu jeshi la polisi lililazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya ili kuweka utulivu katika eneo hilo wakati viongozi wa jeshi la polisi wakiwa katika majadilino ya kutatua kadhia hiyo.

Bonyeza video hapa chini kufahamu kwa kina.