Back to top

Greenwood asaini mkataba mpya kusalia Man United.

16 February 2021
Share

Klabu ya Manchester United imetangaza kuwa mchezaji wao Mason Greenwood amesaini mkataba mpya kuendelea kusalia klabuni humo hadi ifikapo mwaka 2025 huku kukiwa na kipengele cha kumuongezwa mwaka mwingine zaidi endapo mkataba huo utamalizika.
.
Greenwood ni zao la klabu hiyo kutoka katika Academy yake na amekuwa katika klabu hiyo tangu akiwa na umri wa miaka 7.
.
Na sasa akiwa na umri wa miaka 19 amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufunga bao katika michuano ya Ulaya huku akiwa amecheza michezo 82 akiwa na klabu hiyo.
.
Greenwood ni miongoni mwa wachezaji 8 wa Manchester United kutoka academy waliopangwa kwenye timu ya kwanza msimu huu.
.
Mason Greenwood baada ya kusaini mkataba huo amesema kuwa “Pale unapojiunga na klabu hii ukiwa na miaka 7 unakuwa ba shauku ya kucheza katika timu ya kwanza nimepambana sana kufikia hatua hii na miaka miwili iliyopita imekuwa ya mafanikio kwangu  na kuna kila lazaidi ya mafanikio nalolitaka kwenye soka na nafikiri hapa ni mazingira sahihi kwangu kucheza mpira.