Back to top

Guterres agadhabishwa na mapigano yanayoendelea Tripoli.

09 April 2019
Share

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mapigano yanayoendelea mji mkuu wa Libya, Tripoli, ni hatari na ukiukwaji  mkubwa wa haki za binadamu na kuzitaka pande zote zinazopinga na kuanzisha mgogoro kusitisha haraka mapigano hayo.

Bwana.Guterres amekumbusha kwamba hakuna ufumbuzi wa kijeshi katika mgogoro nchini Libya na amezitaka pande zote kushiriki mara moja katika mazungumzo ili kupata suluhisho la kisiasa,amesema hayao katika taarifa Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Uwanja wa ndege pekee ambao umekuwa ukifanya kazi jijini Tripoli ulishambuliwa na ndege za kivita za vikosi vya Marshal Khalifa Haftar, ambavyo vinaendesha mashambulizi mabaya dhidi ya mji mkuu wa Libya.

Tangu Alhamisi, vikosi vya Marshal Khalifa Haftar vinavyodhibiti mashariki mwa Libya vinapigana na majeshi ya serikali ya umoja wa kitaifa inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, na kusababisha watu wengi kupoteza maisha na wengine zaidi ya 3,400 kuyakimbia makazi yao.

Majeshi ya ANL yamekiri kuwa ndege zao ziliendesha mashambulizi dhidi ya uwanja wa ndege wa Mitiga, mashariki ya Tripoli, na kusababisha kusitishwa kwa safari za ndege na abiria pamoja na wafanyakazi kuondolewa.