Back to top

Hakuna mwanadamu aliyeumbwa kwa bahati mbaya - Askofu Njue.

04 November 2018
Share

Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Nairobi nchini Kenya, John Cardinali Njue, amesema hakuna mwanadamu aliyeumbwa kwa bahati mbaya isipokuwa kutekeleza makusudi ya Mungu kwa kutenda mema.

Cardinali Njue amesema hayo Bagamoyo, wakati akizungumza katika maadhimisho ya miaka 150 ya uinjilishaji tangu kuanzishwa kwa Kanisa Katoliki, Tanzania Bara.

Maadhimisho ya miaka 150 tangu kuanza kwa uinjilishaji wa Kanisa Katoliki Bagamoyo, Mkoani Pwani lianza kwa kupiga baragumu na ngoma ikiwa ni ishara ya kuonesha ukristo wa Kiafrika ambapo katika maadhimisho hayo Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ni miongoni mwa waumini waliohudhuria.

Tafsiri ya kupiga baragumu na ngoma, Padre Paul Chiwangu amesema wameanza maadhimisho hayo kwa kupiga vifaa hivyo kama ishara ya kuonesha jambo muhimu katika dini ya Kikristo.

Padre Chiwangu amesema baragumu lilipigwa wakati amri kumi za Mungu zilipokuwa zikipokelewa na kwamba Biblia inaonyesha kwamba ilipigwa wakati wa matukio muhimu ya dini ya kiyahudi.