Back to top

Hali ya hatari yatangazwa kufuatia tishio la Kimbunga Marekani.

12 September 2018
Share

Zaidi ya watu milioni 1.7 katika majimbo matatu upande wa Pwani ya Mashariki nchini Marekani wametakiwa kuondoka katika makazi yao kufuatia tishio la kimbunga kilichopewa jina la Florence.

Gavana wa Jimbo la Carolina Kaskazini Roy Cooper amesema Kimbunga hicho ambacho pia kitayakumba maeneo ya karolina Kusini na Virginia kitakuwa na madhara makubwa huku akiwataka wananchi wake  wasifanye mzaha na maisha yao.

Rais wa nchi hiyo Donald Trump inaelezwa tayari ametangaza hali ya hatari katika majimbo hayo matatu ambayo yatapata mafuriko na uharibifu mkubwa kati ya Alhamis na Ijumaa wiki hii.