Back to top

Halmashauri ya Ilala yaagizwa kuwakata wakandarasi fedha.

18 October 2020
Share

Mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam Mh.Abubakar Kunenge amefanya ziara ya kushtukiza saa saba usiku wa kuamkia leo kukagua miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ikiwemo machinjio ya kisasa ya Vingunguti,soko la kisasa la Kisutu sambamba na stendi mpya  ya mabasi inayojengwa Mbezi .


Ziara hiyo imekuja baada ya Rais wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli kumtaka Mkuu wa Mkoa Dar-es-Salaam kusimamia miradi hiyo kwa weredi.

RC Kunenge ameiagiza halmashauri ya Ilala kuanzia sasa  kuwakata malipo wakandarasi kama fidia ya kuchelewesha kukamilisha miradi ya machinjio ya Vingunguti pamoja na soko la Kisutu ambapo vilitakiwa kukamilika mapema kabla ya kuongezewa muda mwingine.