Back to top

Hatma ya kufunguliwa kwa Shule,vyuo Uganda ni kabla ya Septemba.

21 July 2020
Share

Hatma ya kufunguliwa kwa Shule na vyuo Uganda kuamuliwa kabla ya Septemba,Makanisa na misikiti kuendelea kufungwa.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kwamba ni mapema sana kuruhusu shule na vyuo kufunguliwa au kufutilia mbali kabisa kwa kalenda ya masomo mwaka huu,akiahidi kutoa mwelekeo kabla ya mwezi Septemba mwaka huu.

Shule na vyuo ni miongoni mwa sekta za kwanza kuathirika na marufuku ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Corona.

Museveni anasema kwamba mpango wa kuwapa wanafunzi redio ili kuendelea na masomo ya kidijitali unaendelea,akiwa amwemwagiza waziri wa Elimu ambaye ni mkewe Janeth Museveni na waziri wa fedha kusimamia zoezi hilo.

Kando na Elimu Museveni amesema kwamba makanisa na misikiti itaendelea kufungwa hadi pale mbinu mwafaka ya kuyaruhusu kuendelea na Ibaada itabuniwa.

Marufuku ya kutotoka nje usiku imesongeshwa hadi saa tatu Usiku kutoka saa moja Jioni.

Majengo ya kibiashara maarufu Arcades 110,Maeneo ya vinyozi na kushuka nyweli yameruhusiwa kufunguliwa japo chini ya masharti ya kunakili majina na namba za vitambulisho na za simu za wateja,kuvalia barakoa,kuosha mikono miongoni mwa masharti mengine yaliyotangazwa awali.

Safari za ndege na mipaka itaendelea kufungwa.

Safari za pikipiki maarufu boda boda zitarejelewa kuanzia julai 27,wahudumu na wateja wakitakiwa kuzingatia masharti ya wizara ya afya,ikiwemo kunakili stakabadhi za wateja.