Back to top

Hispania yatakiwa kuacha kuiuzia silaha Saudi Arabia.

18 September 2018
Share

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limeitaka serikali ya Hispania iache kuiuzia silaha Saudi Arabia ili isitangazwe kuwa inashirikiana na Saudi Arabia katika vita inayoendelea nchini Yemen.

Naibu Mkuu wa Masuala ya Kimataifa ya Shirika la Msamaha Duniani la Amesty International STEVE COCKBURN, amesema baada ya miaka mitatu ya vita na uharibifu mkubwa nchini Yemen ambayo maelfu ya watu wasio na hatia wameuawa, hakuna tena kisingizio kwa Hispania cha kuendelea kuuzia silaha muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia.

Shirika hilo limesema Hispani ni nchi ya nne katika orodha ya nchi zinazoiuzia Saudi Arabia silaha, nyingine zikiwa ni Marekani, Uingereza na Ufaransa.