Back to top

Hospitali ya Aga Khan kuchunguzwa kwa kutoza gharama kubwa wagonjwa.

18 February 2021
Share

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema jeshi hilo limepokea malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi ya Hospitali ya Aga Khan ya Jijini Dar es Salaam kutoza gharama kubwa za matibabu kwa wagonjwa wa matatizo kifua (Pneumonia) ambayo hupelekea matatizo ya upumuaji.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam baada kupokea malalamiko hayo limefungua Jalada la uchunguzi lenye kumbukumbu namba DSMZ/CID/PE/34/2021 dhidi ya malalamiko hayo. 

Katika taarifa ya Mambosasa imeeleza kuwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali hiyo, pindi wanapofariki dunia kumekuwa na tabia ya kuzuia miili ya marehemu na kudai kiasi kikubwa cha fedha kinyume na maelekezo ya Serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto.

Ameongza kuwa uchunguzi utakapokamilika na kubaini tuhuma hizo hatua kali za kisheria zitachukuliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto dhidi ya Hospitali hiyo.
 

Attachment: