Back to top

Hoteli ya Bwawani wilaya ya Handeni mkoani Tanga yateketea kwa moto

09 November 2018
Share

Hoteli ya Bwawani ya aliyekua mbunge wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga marehemu Abdalah Kigoda imeteketea kwa moto, ambapo chanzo chake bado hakijafahamika.

Hoteli hiyo imeungua yote na hakuna kilichookolewa, ambapo baadhi ya mashuhuda walikuwepo hotelini hapo  kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya udereva walilazimika kutoka nje kunusuru maisha yao walipoona moshi ukitoka katika hoteli hiyo.

Kwa mujibu wa Afisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  wilayani Handeni Bi. Joani amedai kuwa mpaka sasa bado hawajajua chanzo cha tukio hilo na bado wanaendelea kuudhibiti moto huo usije leta madhala kwenye nyumba za majirani.
 
Kufuatia moto huo Tanesco wamezima umeme katika eneo hilo ili kudhibiti kusije kutokea athari katika maeneo ya jirani na makazi ya watu.

Endelea kufuatilia taarifa zetu kufahamu zaidi.