Kituo cha afya Lupembe wilayani Njombe kinakabiliwa na changamoto ya kukosa umeme kwa takribani mwezi mmoja sasa kutokana na Transfoma iliyokuwepo kuharibika na kusababisha baadhi ya huduma muhimu katika kituo hicho zikiwemo za vipimo na upasuaji kushindwa kutolewa.
Kaimu mganga mfawidhi wa kituo cha afyaLupembe Dkt. Eliud Kibona ameeleza kuwa kutokana na kukosekana kwa nishati ya umeme wanalazimika kutumia mtambo wa mafuta (jenereta) ambao huwashwa kwa muda mfupi na kwamba baadhi ya huduma muhimu zinashindwa kutolewa kituoni hapo .
Akizungumza kwa niaba ya meneja wa shirika la umeme TANESCO mkoa wa Njombe afisa mahusiano wa shirika hilo Bi.Veronica Magoti amesema tatizo hilo linatambuliwa na linatafutiwa ufumbuzi ndani ya muda mfupi.