Back to top

Ibada ya mazishi ya Kofi Annan yanafanyika katika mji mkuu wa Ghana.

13 September 2018
Share

Ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan inafanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

Waombolezaji waliovaa nguo nyeusi na nyekundu wamejaa katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa mjini Accra ambako unaweza kupokea takribani watu 4000.

Watu wengine zaidi wamekaa katika ukumbi mwingine nje ya ukumbi mkuu wakitazama kupitia televisheni shughuli zinavyoendelea.

Wageni waheshimiwa kutoka kote duniania wanahudhuria mazishi ya kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wamataifa akiwemo rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast pamoja na katibu mkuu wa sasa Antonio Gutterrez.