Back to top

Idadi ya maambukizi sasa kufikia 203 Uganda.

16 May 2020
Share

Uganda yatangaza  idadi ya juu zaidi ya maambukizi ya COVID19 chini ya saa 24 na kufanya Idadi ya maambukizi sasa kufikia 203.

Wizara ya afya ya Uganda imetangaza kwamba vipimo kwa sampuli 1838 za madereva waliongia nchini humo chini ya saa 24, 43 tayari walikuwa wameambukizwa homa ya COVID 19 na kuifanya idadi ya juu zaidi kuwahi kuripotiwa tangu nchi hiyo kutangaza kisa cha kwanza.

Miongoni mwa 43 hao 17 ni waganda,14 wakenya,Watanzania 5,raia wa Eriteria 4,raia wa Burundi 2 huku utambulisho wa 1 ukiwa bado haujajulikana.

Sampuli 720 zilizokusanywa kwenye jamii nchini humo hazijaonyesha maambukizi yoyote.

Jumla ya sampuli zilizofanyiwa uchunguzi ni 2558,waliopona wakiwa 63.