Back to top

Idadi ya maambukizi ya Corona Uganda yafikia 160.

15 May 2020
Share

Uganda imethibitisha wagonjwa wapya 21 wa homa ya COVID19 na kufanya idadi ya maambukizi kuwa 160.

21 hao wamebainika baada ya kufanyika vipimo kwa sampuli 1593 za madereva katika mipaka ya Mtukula ,Busia ,Malaba na Elegu.

Sampuli 303 zilizokusanywa ndani ya uganda zimekanusha uwepo wa homa hiyo.

Aidha wizara ya afya yaijatoa maelezo kuhusu ni madereva wangapi wa uganda,kenya na tanzania waliathirika.