Back to top

IGP Sirro asema hakuna haja ya kufunga mipaka.

19 March 2020
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania (IGP) Simon Sirro amesema jeshi hilo limejipanga imara kwenye mipaka ili kuhakikisha kwamba watu wanaoingia nchini wanafuata utaratibu na endapo wakibainika kuwa na viashiria vya virusi vya Corona basi hatua zinachukuliwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Akizungumza na ITV Online IGP Sirro amesema kwa sasa hakuna haja ya kufungwa kwa mipaka lakini kama kutakuwa na sababu ya moja kwa moja vyombo vya usalama vilivyopo katika mipaka vitashauri lakini kutokana na Intelijensia walizozipata hakuna tishio kubwa kiasi hicho mpaka kufikia kufungwa mipaka.

"Sasa elimu tumeshaipata kilichobaki ni sisi watanzania kutekeleza hiyo elimu ambayo tumeipata, manaake ukiipata hiyo elimu, usipoitumia hiyo elimu ukabaki kufanya mambo yako ya zamani mwisho wa siku utaangamiza jamii ya Watanzania" Alisema.

1. Kunawa mikono mara kwa mara.

2. Kutokaribiana sana na mtu mwingine ambaye anakohoa ama kupiga chafya - simama umbali wa mita moja

3. Watu wanaokohoa ama kupiga chafya wasalie majumbani mwao ama kutojichanganya na makundi ya watu

4.Hakikisha kwamba unaziba pua na mdomo unapokohoa kwa kutumia kitambaa ama tishu.

5. Mtu anayehisi joto ama tatizo la kupumua ametakiwa kusalia nyumbani nk.