Back to top

IGP Sirro awaonya viongozi wanaofanya siasa  za ushari.

10 August 2020
Share

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaonya viongozi wa kisiasa nchini kuacha kufanya siasa  za ushari kwa kuzungumza maneno ya ukali wanapoeleza sera zao kwa watanzania.

IGP Sirro amesema hayo katika mahojiano na kipindi  cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV  kila Jumatatu saa tatu kamili Usiku.

Katika hatua nyingine IGP Sirro amewashauri vijana kutojiinga katika masuala ambayo yanafanywa kwa maslahi ya watu wachache kuelekea Uchaguzi Mkuu.