
Serikali kupitia wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa imetoa fidia ya fedha kiasi cha shilingi milioni 243.7 kwa ajili ya wananchi 160 wa vijiji vya choda na mkiwa wilaya ya Ikungi.
Akizungumza wakati wa kikao cha utoaji wa taarifa za mapokezi ya fedha hizo, Mkuu wa wilaya ya Ikungi Bw. Jerry Muro amesema Mheshimiwa Rais ameridhia fedha hizo kutolewa kwa wananchi wa kijiji cha mkiwa na Choda mara baada ya kufanyiwa uthamini na kukamilisha taratibu zote za kisheria za ulipwaji wa fidia.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameishukuru serikali kutekeleza kwa vitendo ahadi ya kuwalipa fidia ili wapishe shughuli za kambi ya jeshi katika kata ya mkiwa wamepongeza mchakato wote wa uthamini kuwa wa wazi na wa ukweli.
DC Muro pia aliwaomba viongozi wa jeshi wanaosimamia kambi ya mkiwa kutumia busara kwa kuwaruhusu wananchi wamalize kutoa mazao yao ambayo waliyapanda katika mashamba yanayozunguka kambi hiyo.
