Back to top

Imani za Ushirikina, waalimu waandika barua waomba uhamisho Mara.

28 May 2020
Share

Wimbi la walimu la kuandika barua za kuomba kuhamishwa kutoka mkoa wa Mara kwenda mikoa mingine limeongezeka kwa kile kinachodaiwa walimu hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ushirikina kutoka kwa jamii inayowazunguka.

Wakati hayo yakijitokeza mkoa huo wa Mara unakabiliwa na upungufu wa walimu zaidi ya elfu nane, huku wilaya ya Musoma, Bunda na Butiama zikiongoza kwa kuwa na matukio hayo.