Back to top

Jacqueline Mengi amewavisha nishani maalum ashindi wa tuzo za I CAN

19 July 2019
Share

Mke wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt.Reginald Mengi, Bi.Jacqueline Mengi amewavisha nishani maalum kama mabalozi wa heshima washindi wa tuzo za mafanikio  ya I CAN, kwenye fani mbalimbali  kwa watu wenye ulemavu mwaka 2019.

Mabalozi hao ambao ni washindi wa tuzo za mafanikio kwa watu wenye ulemavu wamevishwa nishani maalum Jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo Bi.Jacqueline Mengi amesema lengo la hafla hiyo ni kutangaza mabalozi wa tuzo za I CAN na kujadili na kutengeneza mkakati wa kuendeleza kazi na urithi wa Dakta Mengi alioacha kupitia taasisi aliyoianzisha kwa ajili ya watu wneye ulemavu nchini.

Wakizungumza kwa niaba ya mabalozi 16, baada ya kuvalishwa nishani maalum, mabalozi hao, Dakta Hadija Jilala, Mhadhiri Mwandamizi wa tafsiri na taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambaye alitafsiri kitabu cha Dakta Mengi kwa Kiswahili na Bi.Wakonta kapunda ambaye ni mjasiriamali anayetumia ulimi kuandika, wamesema wataenzi na kuendeleza kazi za Dakta Mengi hasa kuhusu watu wenye ulemavu.