Back to top

Jafo amtaka Mtendaji Mkuu wa mabasi ya mwendo kasi kujieleza.

10 October 2018
Share

Waziri wa Tamisemi Mh.Suleiman Jaffo amemuagiza mtendaji mkuu wa wakala wa mabasi ya mwendokasi Bw.Ronald Rwakatare kujieleza mara moja ni kwanini huduma za usafiri zinasuasua na kusababisha adha kwa wakazi wa  Mkoa wa Dar Es salaam 

Pia amemtaka naibu waziri Joseph kakunda kukutana kesho na Menejiment ya DART pamoja na Udart kujua nini kiini cha matatizo yanaukumba usafiri huo.

Aidha amemtaka katibu Mkuu Tamisemi Injinia Musa IYOMBE kuchunguza kama kuna watendaji wa DART wanahujuma mradi huo na wachukuliwe hatua za haraka ikiwemo kusimamishwa kazi.