Back to top

Jafo ataka Stendi Mpya ya Mabasi ya Mbezi Luis kuanza kutumika.

25 January 2021
Share

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe.Selemani Jafo ameelekeza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha Stendi Mpya ya Mabasi ya Mbezi Luis inaanza kutumika muda wowote kuanzia sasa.

Ametoa agizo hilo baada ya kujiridhisha kukamilika kwa miundombinu yote muhimu isipokuwa barabara ya kuingia kituoni hapo ambayo ipo hatua za mwisho.

Hata hivyo Waziri Jafo amemuelekeza Mkandarasi anaejenga eneo la maegesho ya magari madogo kuhakikisha anakamilisha kazi ndani ya wiki mbili kuanzia leo na ametaka taa zifungwe ndani ya wiki moja kuanzia leo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi.Spora Liana amesema kazi zinazoendelea kwa sasa ni Ufungaji wa Viyoyozi, Lifti, ufungaji wa taa na Vifaa vya matangazo, uunganishwaji wa maji kwenye Vyoo na miundombinu mingine ambayo nayo ipo hatua ya mwisho kukamilika.