Back to top

Jamii imetakiwa kuishi kwa kuwajali wenye mahitaji.

04 April 2021
Share

Jamii imetakiwa kuishi kwa kuwajali wenye mahitaji na watoe walichonacho kwa makundi hayo.

Aidha wametakiwa kuwa na upendo kwani Yesu Kristo aliyefufuka ni upendo ni fundisho la upendo.

Hayo yemesemwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi katika ibada ya Pasaka Kitaifa iliyonyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Msimbazi Dar es Salaam.

Leo ni Pasaka, siku ambayo wakristo wanaadhimisha siku ya kufufuka kwa Yesu Kristo baada ya kuteswa, kuuawa na kuzikwa zaidi ya miaka Elfu Mbili iliyopita.

Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One na wafanyakazi wote wa kampuni hizo wanawatakia wananchi wote Heri ya Pasaka.