Back to top

Jenerali Mabeyo asisitiza ushirikiano wa mafunzo kwa majeshi ya Afrika

20 June 2020
Share

Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amesema upo umuhimu wa ushirikiano wa kimkakati wa mafunzo kwa  majeshi ya nchi za Afrika  ili kuimarisha ulinzi wa nchi hizo kiuchumi,kisiasa na kijeshi.

Generali Mabeyo ametoa rai hiyo mara baada ya kutunuku vyeti vya mafunzo ya unadhimu na ukamanda kwa maafisa sitini na tano kutoka mataifa kumi ma mbili ya Afrika waliohitimu katika chuo cha unadhimu na ukamanda kilichopo Duluti mkoani Arusha. 

Mkuu huyo wa majeshi pia akazungumzia mpango wa kuboresha chuo hicho ili kukidhi viwango vinavyohitajika. 

Mafunzo hayo ya kimkakati kwa maafisa hao wa jeshi yametolewa kwa ushirikiano na chuo cha uhasibu cha Arusha.