Back to top

Joe Biden azindua mpango wa ahueni kwa Covid - 19.

15 January 2021
Share

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amezindua Alhamis mpango wa majibu ya virusi vya Corona ambao ni pamoja na kuongeza kiwango cha chanjo na kusaidia kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na janga hilo.
.
The American Rescue Plan utazungumzia kwa kina masuala tofauti, muingiliano usio sawa wa kizazi ambao umezidi kuwa mbaya kufuatia COVID-19, taarifa kutoka timu ya mpito ilisema.
.
Mpango wa Biden, unajumuisha mzunguko mpya wa malipo ya moja kwa moja kwa kaya za Marekani, fedha za kuhamasisha shule kufunguliwa kwa usalama na kuongeza program ya chanjo kitaifa.