Back to top

JPM aishukia TARURA kununua viwanja kujenga majengo kila mkoa.

11 June 2020
Share

Wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) umetakiwa kutumia fedha wanazotengewa katika mfuko wake kujenga barabara badala ya kujenga nyumba kwa ajili ya Ofisi.

Rais Dkt.Magufuli ametoa agizo hilo wakati akifungua jengo la ofisi za makao makuu ya TARURA katika mji wa kiserikali Mtumba mkoani Dodoma.

Rais akaitaka TARURA kutumia majengo ya serikali katika mikoa husika kama ofisi.

Katika tukio lingine Rais ameweka jiwe la msingi la  ujenzi wa barabara kutoka mji mpya wa serikali Mtumba hadi Dodoma na kukabidhi  pikipiki kwa maafisa tarafa 448 ambao wamenunuliwa vitendea kazi hivyo na kufanya maafisa tarafa wote 570 nchini kumiliki vyombo hivyo.