Back to top

jumla ya bilioni 94 zakusanywa kutoka kwa wadaiwa wa mikopo.

15 January 2019
Share

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imekusanya jumla ya TZS 94.01 bilioni kutoka kwa wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu katika kipindi cha Julai – Desemba, 2018 na kuvuka lengo lake la kukusanya TZS 71.4 bilioni katika kipindi hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema leo jijini Dar es salaam kuwa makusanyo hayo yametoka kwa jumla ya wanufaika zaidi 198,659 ambao wamejiari au kuajiriwa katika sekta binafsi na umma.

Ambapo Katika kipindi hicho cha Julai – Desemba HESLB pia imefanikiwa kuwabaini wanufaika wapya zaidi 12,600 ambao walikua hawajaanza kurejesha mikopo yao na sasa wameanza na hivyo kufanya wateja wanaorejesha kufikia 198,656 .