Back to top

Jumuiya ya Afrika Mashariki yazindua sera ya usawa wa kijinsia Arusha.

18 September 2018
Share

Jumuiya ya Afrika Mashariki imezindua sera ya usawa wa kijinsia inayotoa mwongozo wa kusimamia usawa kati ya wanawake na  wanaume katika kushiriki shughuli za maendeleo katika nyanja za kiuchumi na kisiasa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa sera hiyo jijini Arusha Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa Jumuiya hiyo, Marry Makoffu  amesema ushirikiano zaidi katika utekelezaji wa sera hiyo unahitajika, hasa kwa serikali za nchi wanachama.

Mwakilishi wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Ujeruman Joyce Abalo amesema sera hiyo ikitekelezwa na kusimamiwa  vizuri, malalamiko mengi yatapungua na kasi ya maendeleo itaongezeka.

Kwa upande wao, baadhi ya wanawake waliohojiwa na ITV kuhusu sera hiyo wamesema kukosekana kwa usawa wa kijinsia  kumeongeza umaskini katika jamii nyingi za nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na kuendelea kuwepo kwa dhana  kwamba kuna kazi maalum kwa ajili ya wanawake na wanaume dhana ambayo ni potofu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii ya Bunge la Afrika Mashariki Mhe.Abdikadir Omary amesema elimu juu ya usawa wa  kijinisa inahitajika katika jamii kwani wengi wanaamini kuwa inawahusu wanawake pekee.