Jumuiya ya Ulaya imepiga kura kuiwekea vikwazo nchi ya Hungary kwa kile kinachoelezwa nchi hiyo kukiuka misingi ya demokrasia inayofanywa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Victor Orban ambaye hivi karibuni aliweka vikwazo dhidi ya wahamiaji wanaoingia nchini humo, kubana uhuru wa habari na kuweka sheria mpya za uendeshaji wa taasisi za elimu ya juu.