Back to top

Kabudi akabidhiwa kijiti Baraza la Mawaziri SADC

13 August 2019
Share

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amekabidhiwa uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Naibu Waziri Mkuu wa Namibia na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe.Netumbo Nandi- Naitwah aliyemaliza muda wake ikiwa ni sehemu ya mkutano huo utakaohitimishwa na wakuu wa nchi wanachama Agosti 17 na 18, 2019.

Mhe.Netumbo Nandi- Naitwah amemkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi kijiti hicho mapema leo Agosti 13, 2019 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC unaondelea jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Profesa Palamagamba Kabudi amepokea ngao hiyo ikiwa ni ishara ya kuupokea uenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).