Back to top

Kadi ya mpiga kura haitatumika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

10 October 2019
Share

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi kwa wananchi juu ya mazoezi mawili tofauti yanayoendelea nchini ya kuandikisha wapiga kura na kuwatahadharisha kwamba kadi ya mpiga kura inayotolewa na tume haitatumika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwenzi ujao.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Dkt. Wilson Mahera Charles amesema kwamba uandikishaji unaoendelea ambao ulianza tarehe 08, Oktoba 2019 unahusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 24 Novemba 2019 ambao hausimamiwi na Tume bali na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI) kupitia Halmashauri mbalimbali kote nchini.

Aliongeza kwamba mwananchi ambaye hatajiandikisha kwenye uandikishaji unaofanywa na OR-TAMISEMI hatapata fursa ya kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24 mwaka huu.

Aidha, Dkt. Mahera amesema kwamba Tume inafanya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mujibu wa katiba na kwamba uboreshaji huo ni kwa ajili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara utakaofanyika mwakani 2020.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi hilo la kujiandikisha ili wapaete fursa ya kuwachagua viongozi wa mitaa yao siku hiyo ya tarehe 24 Novembe 2019.

Amesema zoezi la uboreshaji wa Daftari lianendelea maeneo mbalimbali nchini kwa mujibu wa ratiba na linawahusu wananchi wenye sifa.