Back to top

Kahawa tani 11.4 yakamatwa ikisafirishwa kimagendo Kagera.

19 October 2018
Share

Kikosi kazi kilichoundwa wilayani Muleba kwa lengo la kupambana na magendo ya Kahawa kimefanikiwa kukamata Kahawa safi yenye uzito wa zaidi ya tani 11.4 iliyokuwa isafirishwe kwa njia ya magendo kwenda nchi jirani kupitia ndani ya ziwa Victoria wakati ikipakiwa kwenye Mtumbwi ambao ni maarufu kwa jina la Maisha service na kuwatia mbaroni watuhumiwa watano waliokuwa wakipakia Kahawa hiyo miongoni mwao akiwemo nahodha wa mtumbwi huo.

Kikosi kazi hicho kimekamata kahawa hiyo  eneo la mwalo wa Katungulu ikiandaliwa kusafirishwa kuelekea Uganda .