Back to top

Kairuki ahimiza matumizi ya lugha rahisi na mitandao ya kijamii.

04 August 2020
Share

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Mheshimiwa Angellah Kairuki amehimiza matumizi ya lugha rahisi na mitandao ya kijamii kufikisha taarifa za masuala ya uchumi na fedha kwa wananchi.

Ametoa rai hiyo katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi, wilyani Bariadi mkoani Simiyu.

Ametaka kampuni za simu za mikononi, tovuti na mitandao mingine ya kijamii itumike kupeleka toleo la Bajeti ya Wananchi kulingana na mahitaji husika ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Aidha, ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) izisimamie taasisi za umma ili zitoe fursa kwa makundi maalum kushiriki katika zabuni za umma kama ambavyo sheria ya ununuzi wa umma inavyoeleza.