Back to top

Kalenda ya msimu wa kilimo kutolewa kwa wakulima.

24 June 2018
Share

Mkuu wa  mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi ameziagiza halmashauri zote za mkoa huo na maafisa ugani kuanzia msimu ujao kuhakikisha  wanatoa kalenda za msimu wa kilimo kwa wakulima na wauzaji wa pembejeo ili kukomesha tabia ya wakulima  kuuziwa viuatilifu wakati msimu  wa kunyunyizia zao husika umepita hali inayochangia kudhohofisha juhudi za serikali kuwakwamua wakulima hasa wakati  huu ambao mkoa wa singida unatekeleza kilimo cha mazao mkakati ya korosho pamba na tumbaku.

Dk Rehema Nchimbi ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na wakulima Maafisa Ugani pamoja na wauzaji wa pembejeo za kilimo  kutoka mikoa ya Singida Tabora Kigoma na Mtawara waliyokutana kupata elimu ya matumizi sahihi ya viuatilifu na mabomba ya unyunyiziaji kutoka Taasisi ya  utafiti wa viuatilifu TPRI  inayolenga kumsaidia mkulima kufanya kufanya kilimo chenye tija.

Kaimu Msajili wa Viuatilifu nchini Habibu Mkalanga anasema wakulima wamekuwa wakipata hasara kutokana kununua viuatilifu visivyo sahihi na kutojuwa wakati wa matumizi hivyo ofisi yake haitatioa vibali kwa wauzaji wasiyo na elimu hiyo.
Wakulima Maafisa Ugani na wauza pembajeo waliyopatiwa elimu ya matumizi sahihi ya viuatuilifu na mabomba ya unyunyiziaji nao wakeleza matarajio yao baada ya kuelimishwa.