Back to top

Kamanda Matei aagiza kujengwa kuta imara katika vituo vyote vya watoto

16 February 2019
Share

Kufuatia sakata la mauaji ya watoto linalotikisa nchi kwenye mkoa jirani wa Njombe, kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Urich Matei ameagiza kujengwa kwa kuta imara kuzunguka  vituo vyote vya watoto yatima katika mkoa huo ili kuwepo usalama wa uhakika kwa watoto wanaopata malezi katika vituo hivyo.

Urich Matei Kamishna Msaidizi wa Jeshi la polisi Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ametoa maagizo hayo  alipokuwa akikabidhi zawadi kwa watoto yatima katika hafla fupi ya kuzaliwa kwa mwandishi wa habari Marry Mwakibete aliyeunda group la whats app  kuhamasisha michango ili kuwasaidia yatima  katika kituo cha Nuru Orphan Center kilichopo Uyole jijini humo.