Back to top

Kambi rasmi ya upinzani Bungeni kuwasilisha Bajeti kuu Mbadala

16 June 2018
Share

Siku chache mara baada ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19 kuwasilishwa bungeni Mwenyekiti wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe amesema kambi hiyo inaona Bajeti Kuu bado haijagusa ukuaji shirikishi wa uchumi ambapo amesema kambi hiyo itawasilisha bungeni hotuba yake itakayogusa maeneo ya vipaumbele ikiwemo sekta ya elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mhe Freeman Mbowe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai amesema Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni imejipanga kuwasilisha hotuba yake huku akidai kuwa bado changamoto kubwa ikitajwa ni utekelezaji wa bajeti inayopangwa katika wizara mbalimbali.

Kwa upande wake Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango ambaye pia Mbunge wa jimbo la Kawe Mhe Halima Mdee amesema kuwa kambi ameyataja maeneo matano ya vipaumbele ambayo kambi hiyo inapendekeza katika bajeti kuu iliyowasilishwa na serikali bungeni.

Serikali inatarajia kukusanya na kutumia sh Trilioni 32.476, ikiwa ni ongezeko la sh Bilioni 764 ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2017/18.