Back to top

Kamishna mkuu TRA akataa hongo ya dola za kimarekani elfu 5.

24 February 2020
Share

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato nchini TRA Dokta  Edwin Mhede amekataa kupokea hongo ya dola za kimarekani elfu tano kutoka raia wawili kutoka China wamiliki wa kampuni ya Longrun International Industrial and Trade ya Mafinga mkoani Iringa walizotaka kumpa baada ya kuomba majadiliano nae kuhusu masuala ya ulipaji kodi ofisini kwake.

Dakta Mhede amesema pia baada ya kufatilia kuhusu kampuni hiyo wamegundua  inatuhuma za kukwepa kulipa kodi ya bilioni  1.375 ambayo ilipaswa kuanza kulipa tarehe 21 mwezi huu.