Back to top

Kampuni ya Tigo yakabidhi zawadi kwa washindi

04 January 2020
Share

Huenda changamoto za Januari zikawa historia kwa baadhi ya washindi ambao wamejipatia fedha kupitia promosheni ya Kishindo cha Funga mwaka kutoka Kampuni ya Tigo (Tigo Pesa) jambo linalowaweka katika nafasi nzuri ya kukabiliana na mambo mbalimbali yanayojitokeza hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka.

“Nilipigiwa simu Jumatano iliyopita nikataarifiwa kwamba ni mshindi wa shillingi milioni 20, kwa kweli sikuamini mpaka nilipoona jina langu katika mitandao ndio nikaamini. Nimshukuru Mungu kwani nilikuwa nina shiriki katika promosheni hii,kwa matarajio ya kwamba na mimi nitaibuka mshindi wa million hata moja,ili niweze kuongeza mtaji,kwa bahati nzuri nimeibuka mshindi wa kwanza wa shilling million 20” ndivyo alivosema Salum Biwi mkazi wa Manzese baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Sh20 milioni Januari 3, 2019.

Biwi ambaye ni mshindi wa kwanza wa Kampeni hiyo alisema ushindi huo ni mkubwa kwake na kwamba amejipanga kutumia fedha hizo kuongeza mtaji kwenye biashara yake ya sasa.

“Mimi nimfanya biashara wa vifaa vya umeme hapa Dar es Salaam na mtaji wangu ni wa kawaida tu lakini kupitia ushindi huu naamini kabisa malengo yangu ya kumiliki biashara kubwa zaidi yatatimia.Nawashukuru sana Tigo kwa kuanzisha promosheni hii kwani ushindi huu utabadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa,” alisema Biwi.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema promosheni hiyo ilifanyika mwezi Desemba kwa lengo la kuwashukuru wateja kwa kutumia huduma ya Tigo Pesa kwa kipindi chote cha mwaka 2019.

“Tunapenda kuwashukuru sana wateja wetu wote ambao walishiriki kwenye promosheni hii lakini kwa leo tumeweza kuwapata washindi watatu ambao wanahitimisha promosheni hii ambayo ilifanyika nchi nzima na tulikuwa na washidi zaidi ya 331 ambao wameshinda milioni 500,” alisema Pesha.

Kwa upande wake Hamidu Mtabiage kutoka mkoani Lindi aliyeshinda Sh15 milioni alisema “Naishukuru sana Tigo Pesa kwasababu mimi ni mfanyabiashara mdogo wa vifaa vya pikipiki na kwa kushinda pesa hizi zitaniwezesha kukuza mtaji wangu kutoka kuuza vifaa hadi kuuza pikipiki kwani hii ni ndoto yangu ya muda mrefu.”

 Naye, Anna Mkongwa aliyeshinda Sh10 milioni, alisema pamoja na kuwa yeye ni mtumishi wa Umma, fedha alizozipata zitamsaidia kutimiza malengo mbalimbali hasa mwanzo huu wa mwaka.

“Kiukweli pesa hizi ni nyingi na sikutegemea kama ningeshinda hivyo kwa sasa nitakachokifanya ni kuweka malengo vizuri na pesa hii itanisaidia kuyatimiza,” alisema Mkongwa mkazi wa Dodoma.

Mbali na washindi hao, Kampeni hiyo ilikuwa ikitoa zawadi kwa washindi 8 wa Sh1 milioni kila siku na washindi 8 wa Sh5 Milioni kila wiki na tayari wamekwisha pokea zawadi zao.