Back to top

Katazo la wananchi kupanda meli mpaka kitambulisho latenguliwa.

21 July 2018
Share

Serikali imelitengua katazo la wananchi kuzuiwa kupanda meli hadi wawe na vitambulisho jijini Mwanza.

Katazo hilo limekuja ikiwa ni siku tatu mfululizo kufuatia vurugu zilizoibuka jijini Mwanza za wananchi kuzuiwa kupanda meli za serikali hadi wawe na vitambulisho.

Akizungumza na  ITV mkoani Njombe  Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi  Mheshimiwa ATASHASTA NDITIYE  amesema suala hilo siyo sahihi na ni uhujumu uchumi.

Mheshimiwa NDITIYE amewataka wananchi waachwe waendelee na safari zao hadi pale serikali itakapokaan kujadili kiini cha tatizo hilo.

Aidha, amewaomba radhi wananchi wa jiji la Mwanza  kutokana na usumbufu walioupata.