Back to top

Katoni 166 za dawa na vifaa tiba zakamatwa Tarakea.

11 September 2018
Share

Shehena ya chakula, dawa na vifaa tiba katoni 166, zimekamatwa eneo la Tarakea, mpakani mwa Kenya na Tanzania, Wilaya ni  Rombo Mkoani Kilimanjaro zikiwa tayari kuingizwa sokoni baada ya kuingia nchini kutoka nje ya nchi kupitia njia za panya bila kukaguliwa wala kulipia kodi.

Mkaguzi wa Dawa kutoka Mamalaka ya Chakula na Dawa, Kanda ya Kaskazini, Bwana FURAHA NYUNZA amesema bidhaa hizo zimekamatwa zikiwa kwenye gari aina ya Fuso Fighter baada ya kuingizwa nchini kinyume cha sheria ya chakula, dawa na vipodozi ya mwaka 2003.

Bidhaa hizo zilizokamatwa ni pamoja na dawa za binadamu, mifugo, vifaa tiba,vitendanishi vya maabara pamoja na vyakula vya kusindika na kwamba mmiliki wa mzigo huo na derva wa gari hilo, mali ya Bwana YUSUSPH SINGANO mkazi wa Tanga walikimbia na kutelekeza mzigo huo.

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi Forodha ya Tarakea, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana ELIAS NJATA amesema thamani halisi ya bidhaa hizo haijajulikana baada ya kukosekana kwa nyaraka za ununuzi kutokana na bidhaa hizo kupitia njia za panya bila kulipia kodi.