Back to top

Kauli ya Rais haikuwa ya kupuuza kanuni za kisayansi za kupambana na C

24 May 2020
Share

Tanzania imeitaka dunia na Jumuiya za Kimataifa kutambua kuwa kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuwahimiza Watanzania kusali na kuliombea Taifa kuondokana na maradhi ya COVID 19 kamwe haikuwa kauli ya kupuuza kanuni za kisayansi za mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema hayo wakati akitoa salam za Shukrani katika Kanisa la Mtakatifu Albano Dayososi ya Dar es salaam,kwa niaba ya Rais Magufuli ikiwa ni hitimisho la siku tatu za kumshukuru Mungu  baada ya maambukizi ya virusi vya corona kupungua nchini

Waziri Kabudi amesema licha ya kauli ya Rais kutaka watanzania kusali bado serikali ilisisitiza kufuatwa kwa kanuni za kisayansi za kuepuka maambukizi ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa,kunawa mikono na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
 
Ameongeza kuwa hatua ya Tanzania kufunga maabara yake iliyokuwa ikipima virusi vya Corona hapo awali kabla ya Rais wa Tanzania kubaini kasoro katika maabara kuu,hatua hiyo iliifanya Tanzania kuchukua hatua ya  kujijengea uwezo wake wa ndani na kujenga maabara mpya yenye uwezo wa kuwapima watu wanaodhaniwa kuwa na virusi vya corona maradufu.