Back to top

Kaya 102 zilizopata maafa ya MV Nyerere zapata msaada wa chakula.

14 October 2018
Share

Tani 15 za chakula cha msaada kwa ajili ya kaya 102 za vijiji vinane vya kisiwa cha Ukara wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza zilizopata maafa ya ajali ya kivuko cha Mv Nyerere  Septemba 20  mwaka huu zimewasilishwa.

Tani hizo za chakula zilizotolewa na Shirika la misaada na maendeleo kwa jamii ADRA zilishindwa kusafirishwa Ijumaa wiki hii kutokana na ubovu wa miundombinu ya bandari ya Bugorola zimewasili katika kisiwa hicho kwa ajili ya kuanza kugawiwa kwa wafiwa.