Back to top

kemikali za kutengeza pombe kali zakamatwa Kagera.

06 December 2018
Share

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika mkoa wa Kagera inalishikilia gari aina ya Benz Actros yenye namba za usajili T. 290 ABC mali ya kampuni ya Atlantic Marketing ya jijini Dar es salaam iliyokamatwa na maofisa wa mamlaka hiyo wakati ikishusha kinyemela wilayani Ngara madumu 128 yenye kemikali za kutengeza pombe kali zenye jumla ya ujazo wa lita 32,000 yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda katika nchi Congo.

Kemikali hiyo ilikuwa ikishushwa kwenye gari hilo na kupakiwa kwenye gari jingine aina ya fuso yenye namba za usajili T. 290 DDG mali ya mfanyabiashara Mseth Suguta mkazi wa Geita ambalo linashikiliwa pia, akizungumza na waandishi wa habari wakati akionyesha magari yanayoshikiliwa na madumu yenye kemikali, meneja wa TRA wa mkoa wa Kagera Adam Ntoga amesema dereva wa gari ambaye amefanikiwa kukimbia na alikuwa akishusha madumu hayo karibu na mpaka wa kabanga ulioko wilayani ngara unaotenga nchi za Tanzania na Burundi.