Back to top

Kenya imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku moja.

11 March 2019
Share

Kenya imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku moja ya raia wake waliofariki katika ajali ya ndege ya shirika la ndege la Ethiopia na kusababisha vifo vya watu mia moja hamsini na saba kutoka nchi thelathini na tano.

Watu thelathini na wawili wa Kenya ni miongoni wa abiria wote 157 waliopoteza maisha kufuatia baada ya ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi nchini Kenya kuanguka.

Ajali hiyo ilitokea mapema jana baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Uwanja wa ndege wa Bore Mjini Adis Ababa.

Taarifa ya awali ya kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines ilisema ndege hiyo ilibeba abiria kutoka mataifa 32 yakiwemo Marekani, Uingereza, China, India, Misri, Canada na Ufaransa.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, ABIY AHMED kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.
Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana.Antonio Guterres, ameelezea kusikitishwa na vifo vya watu hao.

Taarifa ya msemaji wa Bwana.Guterres ametoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa, wakiwemo wale wa wafanyakazi wa umoja huo.

Aidha, ametoa salamu za pole kwa serikali na wananchi wa Ethiopia.