Back to top

Kenya imethibitisha maambukizi mapya 25 ya virusi vya Corona.

04 May 2020
Share

Kenya imethibitisha maambukizi mapya 25 ya virusi vya Corona na kufikisha  490 waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo kufikia sasa.

Wizara ya afya inasema kuwa visa 15 vinatoka jijini Nairobi na 10 kutoka kaunti ya Mombasa.

Wote wakiwa ni wakenya  ambao  hawana historia ya kusafiri nje ya nchi.

Naibu waziri wa afya Dkt Mercy Mwangangi anasema kuwa sampuli 1004 zilifanyiwa vipimo katika muda was aa 24 zilizopita.

Aidha watu 6 zaidi wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha 173 waliopona kufikia sasa.