Back to top

Kenya kufunga mipaka yake.

16 May 2020
Share

Rais Uhuru kenyatta ametangaza kufungwa kwa mipaka yake na mataifa ya Tanzania na Somalia kuanzia usiku wa leo kwa siku 30 zijazo.

Katika hotuba kwa taifa Rais Kenyatta amesema kuwa ni madereva wa magari ya kubeba mizigo pekee ambao ndio wataruhisiwa kuingia nchini Kenya ila tu baada ya kupimwa virusi vya Corona na kupatikana kuwa hawana  virusi hivyo.

Rais Kenyatta akidokeza kuwa amechukua hatua hiyo baada ya madereva wa malori ya kubeba mizigo 78 raia wa kigeni kunyimwa kibali cha kuingia nchini Kenya baada ya kukutwa  na virusi hivyo .

Kenya aidha imeongeza muda wa marufuku ya kutoka nje kwa siku 21 zijazo hadi juni 6.Rais Kenyatta pia ameeleza kuwa kenya imesajili maambukizi mapya 49 ya virusi vya Corona na kufikisha 830 walioambukizwa nchini Kenya.

Aidha idadi ya waliofariki imeongezeka na kufikia 50 baada ya watu watano zaidi kufariki katika muda wa saa 24 zilizopita.

Rais Kenyatta akitoa wito kwa wakenya kuendelea kufuata kanuni ambao serikali yake imekua ikitoa kwa umma kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa COVID 19.