Back to top

Kenya kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya Corona.

21 January 2021
Share

Kenya inatarajia kupokea dozi milioni 24 za chanjo ya ugonjwa Corona iliyotengenezwa na kapuni ya Astrazeneca na chuo kikuu cha Oxford mwezi ujao, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe nchini Kenya amesema kuwa chanjo hizo ziliagizwa kupitia mpango wa Umoja wa Afrika.

Waziri wa mambo ya nje Uingereza, Dominic Raab, ambaye yuko nchini humo kwa ziara ya siku moja, amenukuliwa akisema Uingereza ilikuwa inasaidia Kenya kujitayarisha kuanza kutoa chanjo hiyo.

"Ni wajibu wetu sio tu kimaadili, lakini ni kwa maslahi ya Uingereza kuona raia wa Kenya wakipata chanjo hiyo haraka iwezekanavyo kadri ya uwezo wetu," Bwana Raab amenukuliwa akisema.

Kenya ina idadi ya watu takriban milioni 48, kulingana na takwimu ya idadi ya watu mwaka 2019. Na hadi kufikia sasa nchi hiyo imethibitisha maambukizi 99,308 ya virusi vya corona huku watu 1,130,707 wakifanyiwa vipimo vya virusi hivyo.