Back to top

Kenya yataka uchunguzi kuanguka ndege iliyobeba misaada ya Corona.

06 May 2020
Share

Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya imetaka uchunguzi wa haraka ufanyike baada ya ndege iliyobeba misaada ya kukabiliana na Corona kuanguka Kusini mwa Somalia na kuua watu wote sita waliokuwemo.

Taarifa ya wizara hiyo imetaka serikali ya Somalia ifanya uchunguzi wa haraka na wa kina wa chanzo cha tukio hilo na kuonya kuwa linaweza kuathiri msaada ya kibinadamu inayopelekwa nchini Somalia.

Ndege hiyo binafsi ilikuwa imebeba misaada ya kibinadamu inayohusu janga la Corona wakati ilipoanguka ilipokuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Wilaya ya Bardale Kusini mwa Somalia, kilomita mia tatu Kaskazini Magharibu mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Katika tukio hilo, marubani wawili raia wa Kenya walifariki dunia pamoja na raia wengine wanne wa Somalia, Serikali ya Somalia imesema uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea.