Back to top

Kesi ya Mauaji inayomkabili Mwalimu wa shule ya msingi kusikilizwa leo

15 February 2019
Share

Upande wa Mashtaka katika kesi ya mauaji iliyoanza kusikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Bukoba tangu tarehe sita mwezi huu,  leo unatarajia kufunga ushahidi wa kesi hiyo.

Hayo yameelezwa na Mwendesha Mashitaka mkuu upande wa jamhuri katika kesi hiyo,  Bwana Hashimu Ngole.

Kesi hiyo inamkabili Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kibeta, katika Manispaa ya Bukoba, Respius Patric Rutazangira, anayetuhumiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wa Darasa la Tano katika shule hiyo, Sperius Eradius baada ya kumtuhumu kuwa ameiba mkoba wa mwalimu mwenzake, Alieth Jerard ambaye pia ni mtuhumiwa wa mauaji hayo.

Wakili wa kujitegemea, Bwana Projestus Mulokozi anayewatetea watuhumiwa hao kwa kushirikiana na Bwana Aron Kabunga pamoja Aneth Rwiza, amesema wateja wake wana mashahidi wawili na watatoa ushahidi wao wakati ukifika.