Back to top

Kidato cha nne kuanza mtihani wa Taifa Kesho.

04 November 2018
Share

Bazara la Mitihani la Tanzania limetangaza kuanzia kesho hadi tarehe 23 mwezi huu, watahiniwa wa Kidato cha Nne na  Maarifa wanatarajia kufanya mitihani wa mwisho katika za shule za sekondari Elfu Nne na Mia - Nane na sabini na tatu na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea Elfu- moja na 72 upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dakta Charles Msonde amesema katika  mtihani wa mwaka huu, kuna ongezeko la watahiniwa wa shule zaidi ya Elfu- 44 sawa na asilimia 13.82 na kwa upande wa  watahiniwa wa kujitegemea wamesajiliwa zaidi ya Elfu- 14 sawa na asilimia 55.69 ikilinganishwa na mwaka jana.

Dakta Msonde ametoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa, halmashauri na manispaa kuhakikisha taratibu za uendeshaji  mitihani ya taifa zinazingatiwa ipasavyo ikiwemo mazingira ya vituo vya mitihani kuwa salama.

Kamati zinakumbushwa kuzuia mianya inayoweza kusababisha udanganyifu, pamoja na wamiliki wa shule kutoingilia majukumu ya wasimamizi wa katika kipindi chote cha mitihani.