Back to top

Kifo cha askari polisi aliyefia baa kimeacha maswali Songea.

14 March 2019
Share

Kifo cha askari polisi Donald Motoulaya aliyekuwa akifanyia kazi katika ofisi ya Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma aliyefia katika baa ya Friends Pub iliyoko Songea mkoani Ruvuma usiku wa kuamkia leo kimeacha maswali mengi katika mji wa Songea.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Simon Maigwa Marwa amesema kuwa marehemu kabla ya kifo chake alianza kunywa pombe katika baa ya Yapenda na kisha kwenda baa ya Friends Pub ambako akiwa huko aliteleza na kuanguka na kisha kujilaza kwenye kochi kwa kujipumzisha katika baa hiyo hadi mauti yake.

Kutokana na tukio hilo wananchi wa manispaa ya Songea walikusanyika kuzunguka baa hiyo kushudia tukio hilo .

Kamanda Marwa amesema kuwa mwili wa askari huyo umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa uchunguzi zaidi.